MIAKA MNNE YA UONGOZI WA DKT. SAMIA BANDARI YA DAR ES SALAAM YAONGEZA UFANISI, IDADI YA MELI YAPANDA HADI 1,990
Idadi ya meli zinazoingia katika Bandari ya Dar es Salaam imeongezeka kutoka 1,860 mwaka 2023 hadi 1,990 mwaka huu, hatua inayoashiria ukuaji endelevu wa biashara na ufanisi wa kiuchumi.
Chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, mradi wa Kwala Industrial Park unatarajiwa kuongeza ufanisi mkubwa katika usafirishaji wa mizigo. Safari kutoka Dar es Salaam hadi Kwala zitapungua kutoka siku 45 hadi masaa 30–35 pekee, huku utoaji wa mizigo ukipunguzwa hadi masaa 24.
Aidha, usafirishaji wa mizigo kutoka Kwala hadi Dodoma utachukua masaa 4–5, jambo linalotarajiwa kupunguza utegemezi wa malori, kuokoa muda na gharama, na kuboresha huduma za bandari.
Takwimu zinaonyesha kuwa kupitia ubia kwenye Bandari ya Dar es Salaam, kiwango cha mizigo kimepanda kutoka tani milioni 23.69 hadi milioni 27.76, sawa na ongezeko la asilimia 17