Breaking News

CHINI YA RAIS SAMIA MAUZO YA MADINI YAONGEZEKA HADI USD BILIONI 4.1

Mauzo ya madini nje ya nchi yameongezeka kutoka dola za Marekani bilioni 3.116 mwaka 2020 hadi kufikia bilioni 4.119 mwaka 2024, chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Ongezeko hili limeifanya Tanzania kujiimarisha zaidi kama kituo kikuu cha biashara ya madini katika ukanda wa Afrika Mashariki. Ukuaji huo unatarajiwa kuongeza mapato ya taifa na kuimarisha nafasi ya nchi katika masoko ya kimataifa ya madini.