RAIS SAMIA AIMARISHA SEKTA YA AFYA: ZAHANATI 1,000 NA VITUO VYA AFYA 300 VIMEJENGWA
Chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, sekta ya afya imeimarishwa kwa kasi kubwa nchini. Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya hospitali, vituo vya afya na zahanati imeongezeka maradufu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Mwaka 2020 kulikuwa na hospitali 98, vituo vya afya 433 na zahanati 368 pekee. Kufikia mwaka 2025, idadi hiyo imeongezeka hadi hospitali 150, vituo vya afya 733 na zahanati 1,368. Hii ni sawa na ongezeko la hospitali 52, vituo vya afya 300 na zahanati 1,000 mpya.
Aidha, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba nao umeimarika kutoka wastani wa asilimia 92 mwaka 2020 hadi asilimia 95 mwaka 2025. Ongezeko hilo la alama tatu za asilimia limechangiwa na kuongezeka kwa bajeti ya sekta ya afya, maboresho ya bohari ya dawa pamoja na mikakati ya Serikali kuhakikisha huduma za afya zinapatikana karibu zaidi na wananchi.