RAIS SAMIA AIMARISHA UPATIKANAJI WA DAWA NA HUDUMA ZA KIBINGWA
Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanikiwa kuongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba muhimu katika vituo vya umma nchini kutoka asilimia 73 mwaka 2020 hadi kufikia asilimia 86.2 kufikia Aprili 2025.
Hatua hiyo imewawezesha wananchi kupata huduma bora za afya pamoja na kuvutia wagonjwa kutoka mataifa mengine, ambapo idadi ya wagonjwa waliokuja kutibiwa Tanzania imeongezeka kutoka 5,705 mwaka 2020 hadi 12,180 mwaka 2025.
Aidha, huduma za kibingwa na ubingwa bobezi zimeimarishwa kwa kiwango kikubwa na sasa zinahusisha upasuaji na matibabu ya hali ya juu kama vile: uwekaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto, upandikizaji wa figo, kuwekewa puto tumboni, upasuaji mgumu wa moyo bila kufungua kifua, upasuaji wa moyo kwa kufungua kifua, upasuaji wa ubongo, upasuaji wa uti wa mgongo, upandikizaji wa nyonga bandia, pamoja na tiba ya saratani ya mlango wa kizazi.