Breaking News

RAIS SAMIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU CCM KUTEUA WAGOMBEA UBUNGE NA BARAZA LA WAWAKILISHI

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo, Agosti 21, 2025, jijini Dodoma.

Kikao hicho kimejadili na kufanya uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali ikiwemo Ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge wa Viti Maalum, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Viti Maalum.

Uteuzi huo ni sehemu ya maandalizi ya chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.