Breaking News

RC CHALAMILA AMALIZA MGOGORO WA NYUMBA, AMREJESHEA MJANE BI ALICE HAKI YAKE

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam - Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, amemaliza rasmi mgogoro wa umiliki wa nyumba iliyoko kiwanja namba 819, eneo la Msasani Beach, uliokuwa ukimkabili mjane wa marehemu Justice Rugaobula, Bi Alice Haule, na Bw. Muhammed Mustafa Yusuf Ali.

Katika hafla iliyofanyika leo, Oktoba 20, 2025, Jijini Dar es Salaam, Mhe. Chalamila amemkabidhi Bi Alice hati maalum iliyotolewa na Wizara ya Ardhi, ikithibitisha rasmi kuwa yeye ndiye msimamizi halali wa mirathi ya marehemu mumewe.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mhe. Chalamila alisema aliamua kuunda timu maalum ya wataalamu kutoka ofisi ya Kamishna wa Ardhi, Jeshi la Polisi, na wanasheria kutoka pande zote mbili za mgogoro. Baada ya uchunguzi wa kina, timu hiyo ilibaini kuwa Bi Alice ndiye mwenye haki kisheria ya kusimamia mali hiyo.

“Baada ya uchunguzi wa kina, timu yangu imejiridhisha kuwa Bi Alice Haule ndiye anayestahili kupewa haki ya umiliki wa nyumba hii kama msimamizi wa mirathi ya marehemu mumewe,” alisema Chalamila.
Zaidi ya kumkabidhi hati miliki yenye jina lake, Mkuu wa Mkoa alimpatia Bi Alice kiasi cha shilingi milioni 10 kama kifuta machozi kutokana na usumbufu alioupata wakati wa mgogoro huo. Aidha, alimtaka Bw. Muhammed Mustafa Yusuf Ali kufika ofisini kwake ndani ya siku tano, akieleza kuwa amekuwa akitafutwa kwa muda mrefu bila mafanikio na anatuhumiwa kutumia vibaya majina ya viongozi.

Kwa upande wake, Naibu Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Shukrani Kyando, akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, alifafanua kuwa nyumba hiyo