LOLIONDO COACH YAZINDUA MABUSI YA KISASA KUIMARISHA HUDUMA ZA USAFIRI
Ajenti mkuu wa mabasi ya loliondo coach mkoa wa Arusha akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla hiyo
Mkurugenzi wa kampuni ya mabasi ya Loliondo Coach bwana Chilia John Kimambo (wa kwamza kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi kampuni hiyo.
Mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya mabasi ya Loliondo Coach akigawa keki kwa baadhi ya abiria katika hafla ya uzinduzi wa mabus hayo.
Na Woinde Shizza, Arusha - Kampuni ya usafiri wa mabasi ya Loliondo Coach, yenye makao makuu yake jijini Arusha, imezindua magari mapya matatu ya kisasa aina ya (VVIP Luxury) kwa lengo la kuboresha huduma za usafiri na kuongeza ufanisi katika safari zake.
Akizungumza wakati wa hafla ya utambulisho wa magari hayo mapya, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Chilia John Kimambo, alisema hatua hiyo ni sehemu ya mpango wa kampuni kuhakikisha inatoa huduma bora, salama na za uhakika kwa wateja wake kote nchini.
“Tumeamua kuongeza magari haya mapya ili kuendelea kujibu mahitaji ya wateja wetu wanaosafiri kati ya mikoa mbalimbali,tunataka kila abiria afurahie safari yenye heshima, usalama na starehe,” alisema Kimambo.
Aliongeza kuwa magari hayo yatafanya safari katika njia kuu ikiwemo Arusha–Mwanza, Moshi–Musoma, na Arusha–Loliondo, huku yakitarajiwa kuongeza ufanisi wa huduma na kupunguza changamoto za usafiri kwa wananchi.
Kwa upande wake, Wakala Mkuu wa Loliondo Coach mkoa wa Arusha, Maulidi Rashidi, alisema ofisi kuu za kampuni hiyo zipo katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid, ambapo wateja wanaweza kupata huduma za tiketi na maelezo mbalimbali kuhusu safari.
“Tumejipanga kuhakikisha kila abiria anapata huduma bora kuanzia hatua ya kununua tiketi hadi kufika anakoenda, lengo letu ni kutoa huduma ya mfano katika sekta ya usafirishaji wa abiria,” alisema Rashidi.
Kampuni ya Loliondo Coach imeendelea kujipatia sifa kutokana na ubunifu na uwekezaji wake katika mabasi ya kisasa yenye viwango vya kimataifa, jambo linalochangia kuimarisha usafiri kati ya mikoa ya kaskazini na magharibi mwa Tanzania.







