Breaking News

MCHUNGAJI DKT. NDANSHAU AWATAKA WAUMINI KUMTEGEMEA MUNGU KUPATA AMANI NA UPENDO WA KWELI

Dar es Salaam - Mchungaji Mteule wa Kanisa la Kingdom Impact Christian Centre (TAG) Goba, Dkt Jonathan Chales Ndanshau amewataka waumini wa kanisa hilo waishi katika maisha ya kumtegemea Mungu wa kweli Yesu Kristu ili waweze kuishimaisha ya amani yasiyo na hofu mioyoni mwao.

Dkt. Ndanshau ameyasema hayo katika hafla ya usimikwaji wa kutawadhwa kuwa mchungaji kiongozi wa kanisa hilo uliofanyika leo Aprili 19, 2026 jijini Dar es Salaam.

Amesema waumini hao wakiwa ndani yao na Mungu wa kweli akitawala katika maisha yao watatawaliwa na amani ya kweli, uvumilivu na kupatikana kwa upendo kati yao.

“Sasa hivi kumekuwa na chuki katikati ya wanadamu kwa sababu tofauti zikiwemo ukabila, udini,ukanda wao na milengo ya uongozi lakini Yesu Kristu akiingia mioyoni mwao watapona” amesema
Aidha amefafanua amemshukuu Mungu kwa kuteuliwa na jimbo kuu kwenda kutumikia Kanisa hilo kwa kuonekana anafaa na kazi yake na mzigo wake mkubwa nikwenda kuhakikisha kuona kwamba maisha ya watu wa Goba yanakwenda kubadilika kuboresha katika ulimwengu wa kiroho na kimwili katika maisha yao yote.

Pia alitoa wito kwa Watanzania waondokane na imani za kishirikina na kuacha imani potofu na kuwataka kuishi na Mungu kwakuwa anayeishi na hofu ya Mungu hawataogopa uchawi.

“Mimi kama kiongozi wa dini nawaasa watu wamgeukie Mungu wa kweli wamgeukia Yesu Kristu mfalme wa amani ili waishi kwa raha mustarehe bila hofu, ambapo kwa sasa watu wanaishi kwataharuki ya kuchukuliwa viungo vyao” amesema
Kwa upande wake Askofu Jimbo la Ubungo Asembless of God(TAG) pia Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Kijitonyama ,Ezekiel Mbwilo amewasihi waumini wa kanisa hilo wawe radhi na kutii miongozo ya kimungu ili kuweza kuishi katika njia zilizo salama duniani.

Amesema kinachoihifadhi dunia na ikawaw salama na uponyaji wa kweli kwa mwanadamu upo katika neno la Mungu.

Amefafanua mchungaji Ndanshauni zao zuri lililotengenezwa na Mungu kuwatumikia wanadamu, hivyo Kanisa hilo wamepata kiongozi sahihikatika kuwapeleka watu wengi kwenye ufalme wa Mungu ikiwa na katika kulikuza kanisa hilo kiroho, kiidadi na kuwafikisha watu mbinguni.
“Nawasihi waumini wampokee mtumishi waliyoletewa na Mungu kwa kufanya maombikwa mkuda mrefu, nawahakikishia wamepata mtu sahihi, mlezi na mwalimu mzuri wa kiroho wenye kujitoa katika jamii” amefafanua

Wakati huohuo waumini wa Kanisa hilo wamefurahia ujio wa mtumishi huyokwani walikuwa wakisikia sifa zake alizokuwa akimiminiwa kwa kanisa alilotokea la TAG Kinondoni.Na kabla ya ujio wake mchungaji wa kanisa hilo alitwaliwa na amekwenda mbinguni hivyo wamefurahi kilio chao cha muda mrefu kimepatiwa majibu.