♦️RAHA YA KUWA NA MKE MDOGO KATIKA KABILA LA WADATOGA
Kwa wale ambao dini, taratibu na mila zao zinawaruhusu kuoa wake wengi wakitaka ujuzi zaidi wa namna ya kuishi na wake hao ni muhimu kujifunza kwa kabila la wadatoga linalopatikana katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro kata ya Eyas pembezoni mwa ziwa Eyasi.
Kabila hili ni sehemu ya makabila yanayounda Jiopaki ya Ngorongoro Lengai ambapo makabila mengine yanayounda Jiopaki hiyo ni Wamasai. Wahadzabe na Wairaq ambapo Wadatoga pia ni waumini wa kuoa wake wengi kuanzia wake watatu mpaka wake nane.
Mzee Momoya Maqwel ambaye ni kiongozi wa kabila la Wadatoga anaeleza kuwa inapotokea mwanaume ameoa wake wengi, wanawake hao hupewa majukumu kulingana na umri wao na hivyo mke mdogo ndiye mwenye jukumu la kumlea mwanaume kwani wake wengine huhesabika
kwamba wameshaingia katika rika la uzee.
Mzee Momoya anaeleza kuwa mke mdogo ndio anajukumu la kumlea mwanaume kwa niaba ya wanawake wenzake, inaaminika kwamba mke mdogo anakuwa bado ana nguvu ya kumpa mume huduma zote muhimu ikiwemo huduma ya mapenzi. Huduma nyingine ambazo mke mdogo humfanyia mumewe ni pamoja na kumtafutia chakula, kumpikia. kumuogesha. kumfulia pamoja na mambo yote ambayo mwanaume atayahitaji ili nafsi yake iweze kutulia.
Wakati mke mdogo akiendelea kuvin-jari na mzee.wake wengine huwa hawana wivu wala tatizo lolote kama wanawake wa uswahilini kwani kwa mujibu wa kabila hilo wanawake wote walioolewa na mume husika huwa wanajua kuwa huo ndiyo utamaduni wao na kila mwanaume anapoca mke mdogo yule aliyekuwa mke mdogo.




