POLISI: HAKUNA GARI LA POLISI LILILOCHOMWA MOTO DAR ES SALAAM
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewataka wananchi kupuuza taarifa za uzushi zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa wananchi wamechoma moto gari la polisi mkoani humo.
Katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Julai 4, 2026, Polisi wamesema taarifa hizo si za kweli na zinalenga kupotosha umma pamoja na kusababisha taharuki katika jamii.
Aidha, Jeshi la Polisi limeeleza kuwa linaendelea na uchunguzi wa kisheria na kisayansi ili kuwabaini watu au makundi yanayosambaza taarifa za uongo, na kwamba wahusika watakapobainika watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Jeshi hilo limetoa wito kwa wananchi kuendelea kupata taarifa kutoka vyanzo rasmi na kuepuka kusambaza taarifa ambazo hazijathibitishwa.




