Breaking News

MTANDAO WA WANAWAKE KATIBA, UCHAGUZI NA UONGOZI WASHAURI KUWEPO NA USAWA WA UWAKILISHI KATIKA MAJIMBO YA UCHAGUZI

Mtandao wa Wanawake, Katiba, uchaguzi na Uongozi nchini umeiomba Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuanza kulifanyia kazi suala la misingi ya usawa wa kijinsia lengo likiwa ni mabadiliko ya kisheria yatakayowezesha kufikia uwakilishi wa 50/50 kwa njia ya Majimbo ya uchaguzi ili Wanawake wapigiwe kura na Wapiga kura wote huku pia wakipendekeza Vyama vyote kuhakikisha kama Mgombea Urais ni Mwanaume basi Makamu wake awe Mwanamke na pia Mgombea akiwa Mwanamke Makamu awe Mwanaume.

Akiongea wakati wa kutoa tamko mbele ya Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Kaimu Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na Uongozi, Wakili Victoria Mandari amesema mtandao huo baada ya kufanya uchambuzi yakinifu wa miswada yote mitatu imegundua uwepo wa mapengo ya jinsia katika miswada hiyo.

"Sisi kwa pamoja tunaomba mabadiliko katika miswada ili kuweza kuwa na sheria zenye mlengo mmoja wa jinsia na kuweka misingi ya uwajibishwaji Kwa wale wote wenye dhamana ya kusimamia na kutekeleza sheria husika"

Kwa upamde wake Ananilea Nkya alisema Tafiti zinaonesha kuwa kukosekana kwa Usawa wa Kijinsia kuna changia kwa kiasi kikubwa umasikini na maendeleo hivyo tunaomba Miswada ya uchaguzi ijumuishe 

"Bado kuna ombwe kubwa na Usawa wa Kijinsia bado ni kubwa katika sekta mbalimbali nchi na kupelekea wanawake kuwa nyuma katika sehemu za maamumizi" Alisema Bi. Nkya.