MCHENGERWA: JENGENI UTARATIBU WA KUPIMA AFYA
Waziri wa Nchi ofisi ya rais tamisemi na Mbunge wa Rufiji Mhe. Mohamed Mchengerwa amewaasa wananchi kuwa na utaratibu wa kupima afya kwa maendeleo ya uchumi na ustawi wa familia na Taifa.
Mhe. Mchengerwa amesema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Ikwiriri kwa njia ya video akihitimisha Kampeni Uhamasishaji na utoaji wa Elimu, huduma za Afya na Chanjo katika kipindi cha AFCON 2023.
Akizungumza na wananchi hao waliokuwa wakitazama mechi ya fainali ya AFCON 2023 kati ya Nigeria na Ivory Coast, Mhe. Mchengerwa ametumia jukwaa hilo wakumbusha wananchi hasa wanaume kuwa na desturi ya kupima Afya.
Amesema serikali imewekeza katika sekta ya Afya na inaendelea kuboresha huduma za Afya kwa kusogeza miundombinu ya kutolea huduma,upatikanaji wa vifaa tiba na watoa huduma kuanzia ngazi ya Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali za wilaya.
“Tumefanikisha mambo mengi yanayorahisisha utolewaji wa huduma katika sekta ya Afya ili kuleta Faraja kwa kusogeza huduma kwa wananchi kwa ujenzi wa Hospitali, vituo vya Afya, ujenzi wa zahanati na uletaji wa vifaa tiba hasa katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya sita, ili serikali iendelee kufanya vizuri inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo @uniceftz na mradi wa Breakthrough Action ambao wameamua kuwekeza katika Afya za wananchi”. amesema Mhe. Mohamed Mchengerwa
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele amewaomba wananchi wa Rufiji kuchangamkia fursa zinazojitokeza ikiwemo ya huduma za uchunguzi wa Afya na chanjo bure kwa ajili ya kukinga familia zao na magonjwa mbalimbali ikiwemo ya mlipuko.
Zoezi hili la uhamasishaji Afya kupitia mashindano ya AFCON2023 lilizinduliwa tarehe 17 Januari 2024 na limehotimishwa Februari 11 katika tarafa ya Ikwiriri wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani na lilikuwa likiratibiwa na tamisemi kwa kushirikiana na uniceftz na mradi wa Breakthrough AC







