Breaking News

DKT. MWINYI AWASILI DODOMA KWA AJILI YA VIKAO VYA CCM

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameondoka Zanzibar na kuwasili jijini Dodoma leo kwa ajili ya kushiriki vikao vya kikatiba vya CCM ngazi ya Taifa.

Dkt. Mwinyi alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma, alipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rosemary Senyamule, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, vyombo vya ulinzi na usalama wa mkoa huo.

Vikao hivi vya kikatiba vinatarajiwa kujadili masuala muhimu yanayohusu uongozi na mwelekeo wa Chama hicho tawala.