Breaking News

USALAMA WA NISHATI NI NGUZO YA MAENDELEO – MHANDISI MRAMBA

Arusha - Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, amesema usalama wa nishati ni muhimu kwa usalama wa taifa, maendeleo endelevu na uhifadhi wa mazingira.

Akizungumza kwenye National Security Symposium 2025 jijini Arusha, amesema nishati ni hitaji la msingi, si anasa, na Serikali inaendelea kuwekeza kwenye vyanzo vya nishati safi na ya uhakika.

Kwa sasa Tanzania ina uwezo wa kuzalisha megawati 4,414.69 dhidi ya mahitaji ya megawati 2,316.42, huku asilimia 78.4 ya wananchi wakipata huduma ya umeme.

Ametoa wito kwa sekta binafsi kushirikiana na Serikali kuwekeza zaidi, huku akisisitiza ushirikiano wa kikanda na matumizi ya teknolojia safi kwa mustakabali salama wa nishati.