WAZIRI KOMBO AKUTANA NA RAIS WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU LA KOSOVO
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo amekutana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kosovo, Bw. Agim Ademi pembezoni mwa Mkutano wa Tatu wa Kimataifa kuhusu Wanawake, Amani na Usalama unaoendelea nchini humo.
Mkutano huo ni moja ya mikakati ya Wizara katika kukuza sekta ya michezo nchini kupitia diplomasia ya michezo.





