WAZIRI KOMBO APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA BALOZI MTEULE WA SUDAN
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thatib Kombo (Mb.) amepokea Nakala za Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Jamhuri ya Sudan nchini Mheshimiwa Mohamed Abdalla Abdelhameed Ahmed.
Hafla ya kukabidhi Nakala ya Hati ya Utambulisho ilifanyika tarehe 05 Juni, 2025 katika Ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kupokea hati hizo, Balozi Kombo alisema Tanzania itaendelea kushirikiana na Umoja wa Afrika (AU) na wadau wengine kutafuta suluhu ya mgogoro wa Sudan, kwa njia ya upatanisho na majadiliano ya amani.
Ampongeza Balozi huyo kwa uteuzi wake na kumhakikishia ushirikiano kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Serikalini kwa ujumla; kwa kipindi chote atakachohudumu hapa nchini.
Naye Balozi Mteule wa Jamhuri ya Sudan , Mheshimiwa Ahmed, ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wake katika juhudi za kurejesha amani nchini Sudan na kuwapatia fursa wanafunzi wa Sudan kuendeleza masomo yao nchini, wakati mchakato wa usuluhishi ukiendelea.

.jpg)



