WABUNGE WATANO WACHAGULIWA KUWAKILISHA BUNGE LA AFRIKA
Dodoma - Jumla ya Wabunge watano kutoka Tanzania bara na Zanzibar wamechaguliwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa wawakilishi katika Bunge la Afrika (PAP) katika uchaguzi uliofanyika hii leo Februari 5, 2026 Bungeni jijini Dodoma.
Majina ya wajumbe waliochaguliwa kwa upande wa Wanawake (nafasi moja) ni Lulu Mwacha na upande wa Zanzibar (nafasi moja) ni Imamu Mtumwa Vuai.
Kwa Tanzania bara (nafasi mbili) ni Mariam Mangula na Joshua Nassari huku upande wa kambi yenye watu wachache Bungeni akichaguliwa Rashid Habib Ali.
Aidha, Uchaguzi huo umezingatia uwiano wa idadi ya Wabunge wa vyama vya siasa vyenye wawakilishi Bungeni, uwakilishi wa jinsi na pande mbili za muungano kwa kuzingatia utaratibu wa kanuni za uchaguzi wa Wabunge hao ulivyo katika kanuni za Bunge.
Source Tbc Digital




