Breaking News

TTCL YAZINDUA KITUO CHA KISASA KIDIGITALI “TTCL FTTX EXPERIENCE CENTER”

TTCL imezindua Kijitonyama FTTX Experience Center jijini Dar es Salaam, kituo ambacho kinaonesha uwezo kwa vitendo Intaneti ya kasi ya Faiba inavyowezesha kukuza matumizi ya kidigitali nyumbani, ofisini na hata kwenye biashara.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Bodi, David Nchimbi, amesema TTCL imejipanga kuunganisha Watanzania na dunia kupitia huduma bora za mawasiliano zenye kuwezesha mifumo ya SmartHome na Smartbusiness itakayorahisisha maisha ya kila siku.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu Moremi Marwa ameeleza kuwa kituo hicho ni sehemu ya mkakati wa kuongeza ubora wa huduma na mapato ya shirika, huku kikiwapa wateja fursa ya kujionea ubora wa huduma hizo kwa vitendo.

Tunawakaribisha Watanzania wote kutembelea Kituo cha Kijitonyama FTTx Experience Center waweze kuona kwa vitendo Intaneti yenye kasi Faiba inavyoweza kufanya vitu vingi vya kidigitali