Breaking News

WAZIRI NDEJEMBI AKARIBISHA WAWEKEZAJI WA AFRIKA KUSANI KUJA KUWEKEZA NISHATI TANZANIA

Waziri wa Nishati Mhe Deogratius Ndejembi ametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini na kukutana na Watumishi. Mhe. Waziri Ndejembi (Mb) na Ujumbe wake wapo nchini Afrika Kusini kushiriki Mkutano wa Mawaziri wa Umoja Afrika wanaosimamia Miundombinu na Nishati, utakaofanyika jijini Johannesburg tarehe 30 Aprili, 2026.

Wakati wa mazungumzo Ubalozini, Mhe. Ndejembi (Mb) amewakaribisha Wawekezaji kutoka Afrika Kusini kwenda kuwekeza nchini Tanzania katika uzalishaji wa nishati ya Umeme kutoka Makaa ya Mawe, kama inavyofanyika nchini Afrika Kusini.