JAMIATU AL MUSTAFA YAFANYA KONGAMANO LA 31 LA QUR'AN NA HADITHI
Dar es salaam - Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge ameshiriki katika hafla ya mashindano ya Qur’an Tukufu iliyofanyika eneo la Kigamboni, yakilenga kuhamasisha jamii hususan vijana kujifunza na kuhifadhi Qur’an Tukufu.
Mashindano hayo yameandaliwa na Jamiatu Al-Mustafa ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukuza elimu ya dini pamoja na malezi yenye kuzingatia maadili ya Kiislamu kupitia mafundisho ya Qur’an.
Katika hafla hiyo, washiriki kutoka maeneo mbalimbali walipata fursa ya kuonesha uwezo wao wa usomaji na uhifadhi wa Qur’an mbele ya viongozi wa dini, wazazi pamoja na wageni waalikwa waliohudhuria tukio hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya hafla hiyo, Maulana Sheikh Hemed Jalala alipongeza juhudi zinazofanywa na taasisi hiyo katika kuendeleza elimu ya dini na kuwajenga vijana wenye maadili mema na hofu ya Mungu.
Amesema mashindano ya aina hiyo yana mchango mkubwa katika kuwaweka vijana karibu na dini na kuwasaidia kujenga tabia njema katika jamii
.
Aidha, amewataka wazazi na walezi kuendelea kuwapa watoto wao nafasi ya kujifunza Qur’an na kushiriki katika shughuli za kidini ili kujenga kizazi chenye maadili na nidhamu kwa manufaa ya taifa na jamii kwa ujumla.