TAASISI YA HATUA KWA HATUA NA MAMA YAIVAA CHADEMA, NI KUHUSU BILIONI 2.7
Msemaji wa Taasisi ya Hatua kwa Hatua na Rais Samia, bwana Imani Kayombo akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya hali ya kisiasa nchi na hatua anazochukua tangu kuingia madarakani kwa rais Dokta Samia Suluhu Hassan mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Taasisi ya Hatua kwa Hatua na Rais Samia bwana Amour Abdalla akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari juu ya hali ya kisiasa nchi na hatua anazochukua tangu kuingia madarakani kwa rais Dokta Samia Suluhu Hassan mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Dar es salaam
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo nchini (CHADEMA) kimetakiwa kuwa shukrani kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani kwa hatua yake ya kutoa fedha kwa chama hicho kinachofikia Bilioni 2.7.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Msemaji wa Taasisi ya Hatua kwa Hatua na Rais Samia, bwana Imani Kayombo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali na hali ua kisiasa nchini.
Aidha, Kyombo alibainisha kuwa hatua ya Chadema kutoa maneno yasiyofaa kwa kiongozi wa nchi na kuhamasisha maandamano na kumbeza Rais amedai kitendo kisicho cha uungwana.
"Chadema wawe na shukrani,Rais Samia kupitia maridhiano ameruhusu kutolewa fedha bilioni 2.7 kwa chadema kwa ajili ya kufanya siasa ingetakiwa kupongezwa na Chadema na sio kutoa maneno machafu" Alisema Bw. Kyombo.
Bwana kyombo, aliongeza kuwa Rais Samia ni kiongozi shupavu na anayejali maslahi mapana na kwa Taifa na anayeheshimu uwepo wa vyama vingi ndio maana ameridhia kutoka kwa Fedha.
"Sisi hatua kwa hatua tunampongeza Rais Samia kwa maridhiano mambo ambayo ni sehemu ya Falsafa ya Uongozi" Aliongeza bw. Kyombo





