Breaking News

TLP YAWATAKA WATIA NIA WA URAIS KUDUMISHA AMANI NA UMOJA WA KITAIFA

Dar es Salaam, Mei 26, 2025 — Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Taifa, Richard Lyimo, amewataka watia nia wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar kuenzi na kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.

Akizungumza leo katika Mkutano Mkuu Maalumu uliofanyika jijini Dar es Salaam, Lyimo amesisitiza umuhimu wa wagombea kuzingatia maadili ya uongozi na kutanguliza maslahi ya taifa kabla ya maslahi binafsi. Mkutano huo maalumu umeitishwa kwa ajili ya kumchagua Mgombea wa Urais wa TLP kwa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Mwenyekiti Lyimo amesema chama hicho kitaendelea kuwa jukwaa la kidemokrasia linalotoa nafasi kwa viongozi wenye maono na dhamira ya kweli ya kulitumikia taifa kwa haki na usawa.