Breaking News

DCI KINGAI AFUNGUA MKUTANO WA WAKURUGENZI WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI SADC

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Ramadhan Kingai, leo Juni 4, 2025, amefunga rasmi Mkutano wa Wakurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCIs) kutoka nchi wanachama wa SADC uliokuwa ukifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Mkutano huo muhimu umeweka msukumo mpya katika kuimarisha ushirikiano wa kikanda dhidi ya uhalifu unaovuka mipaka pamoja na kupitia mambo mbalimbali yatakayowasilishwa kesho Jumatano Juni 5, 2025 katika Mkutano Mkuu wa 30 wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka nchi za SADC.