RIDHIWANI AKUMBUSHA UMUHIMU WA CHUO CHA WATUMISHI
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais menejimenti na utawala bora mh. Ridhwani Kikwete (katikati) skiwa na Katibu Mkuu wizara hiyo Bwana Juma Selemani Mkomi( kulia kwake) na Bwana Ernest Francis Mabonesho ambaye ni Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu. Picha na Rajabu Shariffu
Watumishi wa umma nchini wamekumbushwa kuendelea kuzingatia maadili, weledi na uadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao, wakitambua mchango mkubwa wa Chuo cha Utumishi wa Umma katika kuwaandaa kitaaluma.
Rai hiyo ilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhwani Kikwete, wakati wa maadhimisho ya miaka 25 ya Chuo cha Utumishi wa Umma yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mhe. Kikwete alisema chuo hicho kimekuwa na mchango mkubwa katika kuzalisha watumishi waadilifu, wenye weledi na utaalamu, ambapo wengi wao kwa sasa wanashika nafasi mbalimbali za juu za uongozi serikalini, taasisi na mashirika ya umma nchini.
Kutokana na mchango huo, viongozi na watumishi waliotoa huduma na mchango mkubwa katika maendeleo ya chuo walitunukiwa vyeti na tuzo za shukrani kama ishara ya kutambua mchango wao katika maendeleo ya taifa.
Aidha, aliwakumbusha Watanzania umuhimu wa Chuo cha Utumishi wa Umma katika kuendelea kukuza utumishi bora, uadilifu, uzalendo na uwajibikaji kwa manufaa ya taifa.
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali na yalifanyika katika ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam, ambapo wakuu waliowahi kukiongoza chuo hicho pia walitoa nasaha kuhusu umuhimu wa kuendeleza misingi ya utumishi wa umma wenye maadili na weledi.




